Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Yeriko Nyerere Afikishwa Mahakamani Kisutu


Mfanyabiashara na kada maarufu wa CHADEMA   Yericko Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook.

Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184, 2017, Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kuwa mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015

Ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye amesaini bondi ya Sh 10milioni.

Kesi imeahirishwa Juni 5, 2017 kusomewa maelezo ya awali (PH)

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017