Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kaburi La Mtu Mashuhuli Lafukuliwa Uganda

Kaburi la Marehemu, George Kakoma lililofukuliwa

Kaburi la Mtunzi wa Wimbo wa Taifa wa Uganda marehemu, George Kakoma limefukuliwa na watu wasio julikana Jumanne ya wiki hii huku kukiwa na wasiwasi kwamba mabaki ya mwili wake huenda yakawa yameibiwa.

Mtunzi huyo ambaye alifariki Aprili 4 mwaka 2012 na kuzikwa katika kijiji cha Mabwombwe Tarafa ya Mende wilayani Kiso, kaburi lake limeharibiwa na watu ambao hata lengo lao halijafamika mpaka sasa.

Moja ya watu wanaohusika na usimamiaji kaburi na familia ya marehemu aliyejulikana kwa jina la William Kavulu amesema amegundua kaburi hilo kufukuliwa jana asubuhi baada ya kusikia mbwa wakibweka usiku .

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor taarifa zinasema polisi wa eneo hilo na mjane wa marehemu wameomba kibali mahakamani kuweza kuchimbua kaburi hilo, ili kuweza kuthibitisha kama mabaki ya mwili wa marehemu yapo au laa!

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017