Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kesi Ya Kukutwa Na Bangi, Wema Awasili Mahakamani Na Mama Yake

Wema Sepetu akiambatana na mama yake, Mariam Sepetu mahakani hapo.

MLIMBWENDE mwenye jina kubwa Bongo, Wema Sepetu amefika katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo  akiwa na mama yake, Mariam Sepetu na watuhumiwa wenzake wawili kwa ajili ya kusikiliza kesi yao ya kosa la kukutwa na bangi.

Wema, ambaye ni mshiriki wa Shindano la Shepu Bomba linaloendeshwa na Gazeti la Ijumaa ambalo linatoka kila Ijumaa amekana mashataka hayo na hivyo kesi yake kusogezwa mpaka tarehe 1 mwezi wa nane ambapo itaanza kusikilizwa.

Wema Sepetu na mama yake pamoja na watuhumiwa wenzake.

Ikumbukwe kwamba msanii huyo amekuwa na misukosuko mingi ya kufikishwa mahakamani kiasi kwamba watu wengi wamekuwa wakihoji hali hiyo kwani mara kwa mara amaekuwa akifikishwa mahakamani kwa makosa tofauti na ikumbukwe kuwa hata marehamu, Steven Kanumba aliwahi kumburuza msanii huyo kwa kuvunja vioo vya gari lake.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017