Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Lulu Adaiwa Kutoka Na Jaguar


Lulu Diva.
BAADA ya kuweka hadharani kuwa amepata meneja mpya katika za muziki, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kutoka kimapenzi na meneja huyo ambaye pia ni mwanamuziki kutoka Kenya, Jaguar.
Kwa mujibu wa chanzo, hivi sasa mrembo huyo amejiweka kwa Jaguar na hivi karibuni alipewa kipondo na bwana’ke wa zamani baana ya kubaini uhusiano huo.
Jaguar.
“Safari zake Kenya zimekuwa haziishi, wenyewe wanadai wapo kikazi lakini mhh si kwa mapozi ya kimahaba wanayoonesha,” kilibonyeza chanzo na kuahidi kuwabofya picha akiwaona tena.
Baada ya kunasa madai hayo, Star Mix lilimtafuta Lulu na alipopatikana alisema;
“Ni uzushi kama unavyojua Wabongo, Jaguar ni meneja wangu tu ambaye ananisaidia katika kunisimamia katika muziki na si vinginevyo.”

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017