
Rooney akiingia kwenye basi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar.
Mshambuliaji mpya wa Everton, Wayne Rooney amewasili jijini Dar es Salaam akiwa na kikosi hicho kwa ajili ya mchezo maalum ulioandaliwa na SportPesa utakaopigwa kesho kwenye Uwnaja wa Taifa, Dar, dhidi ya Mabingwa wa Sportpesa Super Cup 2017, Gor Mahia kutoka Kenya ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa niMakamu wa Rasi, Bi. Samia Suluhu Hassan

Rooney akielekea kupanda kwenye basi waliloandaliwa wachezaji wa Everton.
Rooney alijiunga na timu hiyo mwishoni mwa wiki iliopita akitokea Manchester United ambapo amesaini mkataba wa miaka miliwi Everton baada ya kuitumikia Man U kwa miaka 13, amerejea katika timu yake zamani ambayo alichezea tangu akiwa kinda.

Hali ilivyokuwa uwanjani hapo baada ya Everton kuwasili.
Nyota huyo wa timu ya taifa England yupo nchini kwa ziara maalum na timu hiyo ambapo ataonekna uwanjani kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Everton kwenye uwanja wa huo wa Taifa kabla ya kurejea England kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa EPL na michuano mingine.
Everton walivyowasili Tanzania.
Rooney anatarajiwa kuwa hamasa kubwa kwenye mchezo huo wa kesjo ambao unasubiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini pamoja na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini


