Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Baraza la habari Tanzania (MCT) Walifufua Upya Sakata la Clouds TV na RC Paul Makonda


Baraza la habari Tanzania (MCT) Jumatatu hii limezindua ripoti mbili juu ya hali ya uhuru wa habari pamoja na tukio la uvamizi wa Kituo cha Clouds Media.


Ripoti hiyo iliyosomwa na mwanasheria mwandamizi Juma Thomas ambaye ni Mwenyekiti wa kamati iliyokuwa na watu wanne, amesema Kitendo cha Makonda kwenda kwenye kituo cha Clouds Media ni kukiuka na kinyume cha Huduma za vyombo vya habari ambapo ripoti hiyo imeweka wazi kuwa Makonda aliingilia uhuru wa Vyombo vya habari na Uhariri wa Habari.

Naye Katibu Mkuu wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema tafiti hizo zinafanywa kama inavyoelekezwa na katiba ya baraza hilo.

“Ripoti hizi mbili zinalenga kuangalia hali ya vyombo vya habari kwa mwaka uliopita kwa maana ya hali ya kiuchumi, sheria, usimamizi,mafanikio pamoja na changamoto,”amesema.

Kuhusu sakata la Clouds amesema lengo la utafiti wa tukio hilo ni kutaka kujua kama lilisababisha athari juu ya uhuru wa habari pamoja na uhuru wa uhariri na si vinginevyo.

“Tafiti zimekuwa zikifanyika tangu mwaka 2001. Wakati alipouawa David Mwangosi tulituma timu ya watafiti, vilevile Serikali ilipozuia matangazo ya Bunge tulifanya tafiti. Kwa hiyo huu ni mwendelezo wa kazi za baraza hili,” amesema.

Amesema tafiti hizo zimehusisha timu ya wataalamu wa sheria, vyombo vya usalama pamoja na wanahabari.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017