Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Cristiano Ronaldo Afungiwa Mechi Tano

Ronaldo akipigwa kadi nyekundu.
Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefungiwa kutocheza mechi tano kutokana na kumsukuma mwamuzi katika mchezo dhidi ya Barcelona, jana usiku.
Shirikisho la Soka la Hispania limemfungia Ronaldo michezo mitano huku moja kati ya mchezo huo ni fainali ya pili ya Super Cup dhidi ya Barcelona.

Akimsukuma refa.
Michezo mingine utakuwa dhidi ya Deportivo, dhidi ya Valencia dhidi ya Levante na wa mwisho utakuwa dhidi ya timu ya Real Sociedad na atarudo mwezi wa 9 kwenye mchezo dhidi ya Real Betis.
Akisikitika.

Mechi 5 ambazo Ronaldo atazikosa;
Barcelona- 16 Agosti
Deportivo- 20 Agosti
Valencia- 27 Agosti
Levante- 9 Septemba
Real Sociedad- 17 Septemba

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017