Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) laonywa jinsi lilivyomaliza mgogoro wa Makonda na Clouds.

Kufuatia maoni ya baadhii ya watu mbalimbali na waandishi wa habari kutoridhika na maamuzi ya Jukwaa la Wahariri (TEF), viongozi wamepewa onyo la kutorudia makosa baada ya kukiri.

Katika mkutano mkuu uliofanyika Agosti 13, viongozi hao walikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari Agosti 9 bila ya kupata idhini.

Hatua hiyo ilisababisha kujengeka kwa taswira mbaya kiuwajibikaji, kanuni na utaratibu.

Katika taarifa ya Mwenyekiti Maalum wa TEF, Walace Mauggo imeeleza kuwa jukwaa kwa kauli moja limetoa onyo kwa viongozi wake kutorudia yale ambayo yamejitokeza.

“Baada ya kutafakari na kutathmini mwenendo wa mkutano huo, jukwaa lilobaini kuwepo kwa kasoro kubwa wakati wa kurejesha mahusiano wa kikazi na kiongozi ambaye habari zake zilizuiwa kuripotiwa kwa takribani miezi mitano,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia wametakiwa kuhakikisha kunapotokea masuala makubwa kama hayo ambayo yashafanyiwa maamuzi na mkutano mkuu na taasisi nyingine za habari yanarudiswa maamuzi kwa wanachama kabla ya hatua za  mwisho.

Mauggo ameeleza kuwa TEF haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi au mtu yoyote atakayeonekana kutishia usalama wa wanahabari, uhuru wa uhariri na vyombo vya habari.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017