Watu wawili wameuawa wakati wa vurugu wakikabiliana na maofisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare, Mji Mkuu wa Nairobi nchini Kenya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa walisikia milindimo ya risasi zikifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo ambayo yalisababisha vifo hivyo.
Afisa Habari wa Shirika la Habari la Ufaransa, Agence France-Presse (AFP), limeeleza kuwa, waliouawa walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji katika eneo hilo ambao walikuwa wakipambana na kikosi maalum cha kuzuia ghasia hizo.
”Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi”, alisema ofisa huyo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.
, Saa Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa
Katika matokeo ya awali ya vituo 39091 kati ya 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:
- Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,977,905 (54.32%)
- Raila Odinga wa ODM ana kura 6,578,586 (44.79%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 387,959.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini