Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Al Shababu Waua Watu 12 Kwa Shambulio La Bomu


Shambulizi la bomu lililotekelezwa na kundi la Al – Shaabab, limesababisha vifo vya watu 12 wakiwemo wanajeshi watano katika mkoa wa Puntland.

Shambulio hilo limetokea leo katika eneo la Af – Urur lililopo karibu na milima ya Galgala kilomita 100 kusini mwa mji wa Bossaso, eneo ambalo linadhibitiwa na Al – Shaabab ambapo mwezi Juni waliuwa watu 38.

Al – Shaabab ambalo linahusishwa na mtandao wa kigaidi wa Al – Qaeda limekuwa likitekeleza mashambulizi nchini likipinga serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na kutaka kuweka utawala wa sheria za Kiislaam.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017