
Hamisa Mobetto.
MAMA mzazi wa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto anayedaiwa kuzaa na msanii wa Bongo Flava, amecharuka akisema kuwa, japokuwa mtoto wake huyo anapigwa vijembe, lakini kamwe hawatamsikia akisema kwa sababu amemwambia afunge mdomo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mama Mobetto alisema kuwa, yeye kama mama anasikia uchungu kuona mwanaye huyo anavyosengenywa, lakini kwa busara amemtaka kutofungua mdomo kujibizana na mtu yeyote kuhusiana na ishu hiyo.
“Hamisa hatafungua mdomo kuzungumza chochote kuhusiana na mtoto wake na siyo mjinga kunyamaza, ila tu hatutaki malumbano na mtu,” alisema mama Mobetto.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini