Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Uchawi Unaotumika Kummaliza Kisanii Diamond Platnumz Wagundulika.....


Msanii wa kimataifa ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya WCB Diamond Platnumz hatimaye uchawi unaotumika kumshusha na kummaliza kabisa kisanii wagundulika.

Katika utafiti nilioufanya kwa miezi kadhaa hatimaye nimegundua kuwa kitendo cha diamond kulinganisha kazi zake za kimuziki na wasanii aliowazidi kimafanikio na kiuimbaji hasa huyu Ali kiba kinamrudisha nyuma sana diamond wakati huo huo mpinzani wake anafaidika sana kupitia mchuano huo ndio maana hataki bifu lao liishe.


Miaka kama miwili mitatu iliyopita diamond alipiga hatua kubwa sana za kimuziki mpaka akawashtua wasanii wakubwa duniani kama vile Chris Brown, Nelly, Neyo,Jiddena,Trey Songz,na wengineo wengi sana.

Na kikubwa kilichomfanya diamond kupiga hatua hiyo ni kitendo cha yeye kutoshughulika na wasanii wa kitanzania badala yake alipenda kulinganisha uwezo wake na wasanii kutoka nchi zingine hasa Nigeria.

Na mpinzani wake mkubwa kutoka Nigeria alikuwa David Adeleke Adedeji (DAVIDO) na kiasi kikubwa ilimsaidia diamond kujulikana sana Nigeria mpaka mashabiki wa muziki wengi walimtambua diamond kama msanii kutoka Nigeria.

Kipindi hichohicho pia Kenya walikuwa walishaanza kumtangaza Diamond kuwa ni msanii kutoka nchini kwao na kudai kuwa uthibitisho wanao.

Lakini kitendo cha Diamond kurudi nyuma na kulinganisha kazi zake na Ali Kiba kama hapo awali kimemrudisha nyuma sana Diamond na thamani yake halisi imeanza kufifia.


Rai ; Nikiwa kama shabiki nguli wa diamond napenda sana kumhusia aachane na Ali kiba , Kiba anatembelea nyota ya diamond kwa sasa na anaitumia kama daraja ili kuweza kuzivusha kazi zake za kimuziki mbali zaidi huku yeye diamond akizidi kufifia kimuziki.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017