Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Wakati Tunashabikia ya Kenya,Tanzania Haina Jaji Mkuu zaidi ya Miezi 8


Hakika Tanzania ni inatakiwa iingie kwenye vitabu vya kumbukumbu kama nchi ya maajabu duniani

Wakati wanatanzania wanashabikia na kukesha mitandaoni wakijadili demokrasia ya Kenya,wao hata Jaji Mkuu wa kutoa maamuzi mazito kama hayo hawana.

Licha tu ya kutilia mashaka upatikanaji wa Jaji huyo Mkuu lakini hata uwepo wake tu umekuwa kizungumkuti.

Watanzania wengine wanahoji mbona wapinzani hawakwenda mahakamani kupinga uraisi wa JPM?

 Wenzetu Kenya wamepigania katiba yao na kuapa kuisimamia. Mihimili yao nimekuwa huru kufanya maamuzi.

Njoo hapa kwetu ! Uliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anateuliwa na nani, Kamishna anatueliwa na nani, Jaji anateuliwa na nani?

Na hali inavyoendelea hivi hakuna aliyedhubutu kunyanyua mdomo, ukiacha wachache kama kina Tundu Lissu ambao wamejitoa bila kujali chochote

Naona Vingozi wengi wa TZ jana wamefunguka kuzungumzia mambo ya Kenya wakati ya kwenu yamewashinda na hamuwezi hata kuzungumzia tu?

Ulishawahi kuona wapi nchi ya Kidemokrasia,Wananchi wanaiogopa serikali?
Serikali ndio inatakiwa kuwaogopa wananchi.

By OKW BOBAN SUNZU/Jamii Forums

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017