BAADA ya kugoma kuuzika sokoni tangu likamatwe, yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa, hatimaye lile gari aina ya Range Rover Evoque 504 lililokuwa likimilikiwa na Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, limeuzwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa, gari hilo liliuzwa hivi karibuni na aliyenunua ni kigogo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa).
“Unajua gari la Wema limesota sokoni kwa muda mrefu sana na lilikuwa likipigwa mnada na Kampuni ya Yono Auction mara kadhaa ila lilikuwa likigoma. Lakini hivi karibuni kwenye mnada lilipata mteja ambaye ni mfanyabiashara huyo maarufu,” kilisema chanzo hicho.
Mara kadhaa magazeti yetu yamekuwa yakiripoti kuhusu gari hilo kugoma kuuzika kutokana na kwamba wanunuzi waliokuwa wakijitokeza walikuwa hawafikii bei waliyokuwa wamepanga kuliuza TRA na kusababisha gari hilo kuchakaa likiwa ‘yard’ kabla ya kupata mteja huyo wa sasa.
Novemba Mosi, 2015, Wema aliangusha bethidei ya nguvu na kujizawadia gari hilo, lakini miezi michache baadaye lilikamatwa na TRA kwa sababu liliingizwa nchini bila kulipiwa kodi. Mmoja wa maofisa wa Yono ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, alithibitisha kulipiga mnada gari hilo baada ya kupata ‘tenda’ kutoka TRA.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini