Imamu wa Msikiti wa Al Masjid Kirumbi Islamic Center uliopo Kimara amewazuia waumini wake kutoshiriki katika kuvunja au kutoa kitu chochote katika msikiti huo ambao unatakiwa kuvunjwa na Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS.
Imamu wa Msikiti huo Ramadhan Juma amesema hayo jana wakati akifanyiwa mahojiano na MCL na kudai kutokana na imani yao ni kosa kubwa mtu yoyote kuvunja nyumba ya ibada kwa kuwa hiyo ni nyumba ya Mungu na kusema wao hawajatoa kitu chochote zaidi ya vitu vidogo ambavyo vinatumika kusaidia jamii kama jeneza.
"TANROADS wametupa barua ya kuvunja msikiti ndani ya wiki moja kwa kile wanachodai umevamia eneo la barabara hivyo walitaka tutoe vifaa ndani ya wiki moja kupisha zoezi la barabara lakini kutokana na imani yetu na Uislam unavyotufundisha ni kosa kubwa kuvunja nyumba ya 'Allah Subhanahu Wa Ta'ala'
"Hii ni nyumba ya ibada hivyo hatutainua mikono yetu kwa kujihukumu sisi wenyewe kwa amri ya dini yetu ya Kiislam kwetu sisi ni kosa mtu kutoa mkono wake kutoa sijui bati au chochote kile kinachohusu msikiti kwa hiyo ndiyo maana tumeshindwa kuvunja msikiti huu" alisisitiza Imamu Ramadhan
Hata hivyo Imamu alisisitiza kuwa wao wameiachia serikali na hao TANROADS waweze kubomoa wenyewe na kusema yeye amewakataza waumini wake wasishiriki cha chochote katika kubomoa nyumba hiyo ya ibada
"Nimewaambia waumini wangu wasitoe chochote katika kuvunja kwa msikiti huu, tutatoa vitu vidogo vidogo ambavyo vinasaidia jamii kama vile jeneza na vinginevyo tumevitoa lakini katika majengo kwa chochote kile tunawaachia wenyewe, hii ni nyumba ya Allah hivyo wavunje wao halafu Mungu mwenyewe ndiye atajua kwa kuwa hiyo ni nyumba yake atakavyohukumu yeye ndiye anajua kwa kuwa hiyo ni nyumba yake" alisema Imamu Ramadhan Juma
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini