KESI inayomkabili muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, imeendelea kusikilizwa leo Jumatatu, Oktoba 23, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa nne upande wa Jamhuri anatoa ushahidi wake.
Katika ushahidi huo imeelezwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Binadamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dtk. Innosent Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa kesi hiyo, aliletewa oda kutoka Jeshi la Polisi kwamba aufanyie uchunguzi mwili wa Steven Kanumba uliokuwa mochwari akishirikiana na daktari mwingine.
“Tulifungua ubongo wa Kanumba na kuukuta umevimba, mishipa midogomidogo ya ubongo ilikuwa imeingia damu, lakini kabla ya kufungua ubongo, kwenye kisogo kulikuwa na mgando wa damu.
“Baada ya kumaliza uchunguzi wetu tulipeleka sampuli kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo tulipeleka pia sampuli mbalimbali za viungo vya mwili wake,” amefafanua Dkt. Mosha.
Ushahidi bado unaendelea kutolewa mahakamani.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini