Muigizaji wa filamu bongo Shamsa Ford amemuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, na kumtaka alegeze kidogo kamba ili hali ya maisha ikae sawa kiuchumi.
Kwenye ukurasa wake wa instagram Shamsa ameandika ujumbe akisema hali siku hizi imekuwa ngumu kiasi cha watu kushindwa kufanya yale waliyoyazoea kwenye maisha yao ya kila siku, hata biashara imekuwa ngumu zaidi, na kama kunyooka ilipofikia imetosha.
"Mr President tunaomba ulegeze kidogo hali mbaya baba, tumeshashika adabu sasa hivi na tunaheshimu pesa .Buku sasa hivi tunaiita elfu moja, yaani sijapata hata mialiko ya birthday kubwa kubwa kama ambavyo wanafanyaga. Mbwembwe hakuna tunaishia kupostiana instagram tu.
Baba naomba usikie kilio changu hali mbaya sitaki kurudi iringa kulima mjini patamu jamani. Biashara imekuwa ngumu sana wateja hakuna jamani ...Baba Tuonee huruma jamani tumepauka kweli yaani mpaka ukimuona mwenzio unakimbia", ameandika SHamsa Ford.
Shamsa Ford ambaye kwa sasa ameolewa na mfanya biashara maarufu hapa mjini, amekuwa kimya kwenye sanaa kwa kutotoa kazi mpya kama ambavyo alizoeleka, hali inayozidi kuibua sintofahamu kama inasababishwa na ukata ama la.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini