Wanasema ni bora ukose kingine chochote lakini sio habari zinazoendelea ulimwenguni sasa hivi ikiwemo hii iliyotokea kwa Rais Mugabe huko Zimbabwe.
Kuna Muhubiri anaitwa Philip Mugadza ambae alitabiri siku kadhaa zilizopita kwamba Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (93) atafariki October 17 2017.
Alisema hicho ni kitu alionyeshwa na Mungu lakini saa kadhaa zilizopita Muhubiri huyo amejitokeza tena hadharani na kusema Mugabe hatokufa tena October 17 kama ilivyopangwa, Mungu ameahirisha mpaka tarehe nyingine.
Mugadza amenukuliwa akisema “siku tatu zilizopita nimepokea neno kutoka kwa Mungu akisema kifo cha Mugabe kimeahirishwa mpaka tarehe nyingine ambayo haijatajwa, sio kwamba nimekua nikisali ili afe ndio nionekane mkweli bali hili ni neno la Mungu na lazima nilifikishe kama lilivyo“
Kwa upande wa Serikali ya Zimbabwe, Waziri wake wa habari alionekana kucheka kuhusu utabiri wa Mugadza na kusema Rais Mugabe mwenyewe ni Mkristo na amekua akimuabudu Mungu, hawezi kuwa na wasiwasi hata kidogo na utabiri unaofanywa na watu.
Waziri Simon Khaya Moyo amesema Serikali ya Zimbabwe haikupata wasiwasi wowote kwenye utabiri huo na kwamba kazi zimeendelea kama kawaida, itapendeza tu kujua Muhubiri huyo ndio atakufa lini.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini