Shirika la afya duniani (WHO) limemteua rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kuwa balozi wa kuunganisha vita ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza barani Afrika.
Kuteuliwa kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 kumewashangaza wanachama wengi wa shirika hilo pamoja na wafadhili hasa kutokana na hali ya sekta ya afya nchini Zimbabwe.
Wanachama wengi na wafadhili wa shirika la afya duniani wamedai kuwa chini ya uongozi wa rais Mugabe sekta ya afya nchini Zimbabwe imezorota huku wafanya kazi wakiwa hawalipwi ipasavyo na dawa pia hazitoshi jambo ambalo linaonyesha kuwa Mugabe hakustahili kupewa wadhfa huo.
Upande wa upinzani chini Zimbabwe umeuita uteuzi huo kuwa vichekesho na matusi kwani kiongozi huyo ameshindwa kuhimarisha sekta ya afya nchini kwake wakati yeye na familia yake wakitibiwa nje ya nchi.
Hata hivyo kiongozi mpya wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus kutoka Ethiopia ambaye ni mwafrika wa kwanza kuongoza shirika hilo alipongeza juhudi za Zimbabwe kwa kujitoa kuboresha afya za wananchi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini