Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi ameshiriki zoezi la uvunjaji wa nyumba kwa kuvunja nyumba yake kwa hiari iliyokuwa imejengwa ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi wa barabara.
Waziri Lukuvi amevunja nyumba yake iliyokuwa imejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara kuu iendayo katika hifadhi ya Ruaha katika Kijiji cha Mapogolo, mkoani Iringa.
“Kama kiongozi nimeamua kuonyesha mfano kumuunga mkono Mhe. Magufuli ambaye ameamua kuiboresha barabara hii kuwa kiwango cha lami mpaka Ruaha National Park ili kuongeza mapato ya nchi lakini pia kuongeza vipato kwa wananchi wa barabara hii wanayoitumia”.
“Kwa faida hizo nimeamua mimi mwenyewe kuvunja leo hii nyumba ili wananchi wa eneo hili ambao barabara hii itajengwa lazima wahakikishe wanabomoa wenyewe nyumba zao,” alisema Waziri Lukuvi.
Aidha Waziri Lukuvi aliwataka wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuzivunja wenyewe nyumba zao ili kurahisisha zoezi la upanuzi wa barabara hiyo uwe wa muda mfupi, kwani barabara hiyo inajengwa kwa manufaa yao.
“Lazima tutii sheria bila shuruti. Tuliowekewa alama ya X tuvunje nyumbza zetu ili kazi ya ujenzi wa barabara hii iwe nyepesi, gharama iwe ndogo na iende kwa muda mfupi,” alisema Waziri.
Vilevile aliwakumbusha wakazi wa eneo hilo ambao wamejenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kuwa wasitegemee fidia yoyote kutoka serikalini na badala yakee waanze kuzibomoa nyumba zao pasipo kusubiri kuja kubomolewa kwa nguvu.
“Serikali haitolipafidia kabisa kwa watu waliojenga kwenye eneo la barabara kama mimi,” alisema.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini