Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Albert Msando Afunguka Kuhusu Video Yake na Gigy Money Wakiwa Kwenye Mahaba Mazito

Albert Msando Afunguka Kuhusu Video Yake na Gigy Money Wakiwa Kwenye Mahaba Mazito
MWANASHERIA maarufu nchini aliyekuwa Chama cha ACT Wazalendo na hivi karibuni akahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Albert Msando, kwa mara ya kwanza amefunguka LIVE kuhusu video yake akiwa na mwanamuziki na modo Gigy Money iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwezi Mei mwaka huu.


Video hiyo ilimuonyesha Msando na Gigy Money wakiwa ndani ya gari, huku Msando akipitisha mkono wake juu ya mwili wa Gigy, wakati huo Gigy Money akikata kiuno huku anacheza muziki.
Akifanya mahojiano leo  kwenye Kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa kupitia Clouds TV, Msando amesema;

“Kuhusu video na Giggy sikuwa namfahamu na kusema kweli tukio lile lilitokea wakati nimekunywa pombe,  sikuwa namfahamu Giggy na hata juzi nilikutana nae kwenye ndege sikumkumbuka.

Ile ni moja kati ya sehemu zilizonisaidia katika maisha yangu, ilinisaidia kujua jamii inanichukuliaje na nini inategemea kutoka kwangu. Video ile haikutengenezwa kwa sababu zozote, mimi sikuwa namfahamu Giggy.

“Tukio lile lilitokea wakati nimekunywa kilevi, sikuwa nikitambua kilichokuwa kinaendelea. Zaidi ameeleza kuwa video ile ni funzo kwa jamii nzima kuwa responsible hata kama hujakamatwa, usisubiri uwe ‘caught on camera’ ili uwajibike,” alisema Msando.

Hata hivyo, baada ya video hiyo kusambaa watu mbalimbali walionyesha kuchukizwa na wanavyomfahamu Mwanasheria Albert Msando mtu wanayemwona ana  heshima kubwa na umaarufu katika jamii,  ambapo aliomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kuhusu kuacha kusimamia kesi ya wema Msando Amesema “Niliacha kuwa Wakili wa Wema Sepetu baada ya Kibatala na Lissu kuanza kumtetea, bado ni mshikaji wangu, na nimekua nikiona hiyo habari inayozunguka kuhusu Wema Sepetu kujiandaa kurudi CCM, namkaribisha” 
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017