Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Habari Mpya Kutoka Simba Leo Alhamisi


Klabu ya Simba ya jijinni Dar Es Salaam ambayo siku kadhaa ilisafiri kutoka jijini Mbeya mpaka mkoani Katavi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Nyundo ya mkoani humo na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana wameamua kubadili mipango yake juu kwa Juu.

Simba   kupitia kwa Mratibu wake Abbas Ally amesema  kuwa Simba wangecheza mchezo wa kirafiki leo Alhamis na Timu ya Rukwa Fc ya Sumbawanga katika uwanja wa Nelson Mandela na Kisha Ijumaa timu ingerejea Mbeya kuendelea na kambi ya maandalizi ya Mechi dhidi ya Prisons.

Lakini kwasasa kunamabadiliko kwani Simba licha ya Kufika Sumbawanga watakaa Sumbawanga mpaka Jumamosi ndipo watacheza na Rukwa Fc kisha baada ya mchezo huo watarejea Mbeya walipokuwa awali.

Simba inatarajia kufanya mazoezi yake katika uwanja wa Nelson Mandela uliopo mjini Sumbawanga mpaka Siku ya Mchezo huo wa kirafiki.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017