Kamanda Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewafikisha katika Mahakama ya Jiji, watuhumiwa 95 kujibu tuhuma za kuwaibia na kuwabugudhi na kuwaibia wasafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa alisema, kati ya watuhumiwa 106 waliokamatwa katika oparesheni iliyofanyika alfajiri ya Novemba 8, 2017 saa 11.00, watuhumiwa 95 walikutwa na makosa ya kubughudhi abiria, kuibia abiria, kuuza tiketi zisizo halali (bandia) na kujivalisha sare za mawakala wa mabasi wakati wakijua kwamba siyo mawakala wa mabasi husika.
“Aidha watuhumiwa wengine 11 baada ya uchambuzi walibainika kuwa na kesi mbalimbali zinazoendelea na wamepelekwa Kituo Kikuu cha Magomeni kuendelea na tuhuma zinazowakabili. Msako huu utakuwa endelevu katika Stendi za Mbezi, Temeke na vituo vyote vya mabasi ya abiria na mizigo,” alisema Mambosasa.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini