Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Lamar : “Mziki Wa Bongo Ni Kama Huu Wanao Fanya Diamond Na Allykiba

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema muziki wa Bongo Flava umekosa utambulisho ukilinganisha na ule wa Nigeria, sasa Bongo5 tumemtafuta Producer Lamar kuzungumzia suala hilo.
Producer huyo kutoka studio za Fish Crab amesema si sawa kusema muziki wa Bongo hauna utambulisho na kila msanii ana kitu chake ambacho kinatambulisha kuwa muziki husika unatoka Bongo.
“Kwanza huyo anayesema muziki hauna utambulisho hathamini cha nyumbani kwa sababu muziki wetu una utambulisho, unajua kila muziki una utambulisho wake ila unajaribu kuchukua vitu fulani kutoka sehemu fulani kuleta ladha tofauti, so ukisema muziki wetu hauna utambulisho unakosea sana” amesema.
“Kina Diamond wana identity zao, kina Alikiba na wasanii wote wanaofanya hip hop, Bongo Flava wana utambulisho wao, unajua kabisa huu muziki unatoka Bongo” ameongeza.
Lamar ameshafanya kazi na Diamond katika ngoma ‘Moyo Wangu’ na Alikiba kupitia ngoma ‘My Everything’.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017