Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa si kweli kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli anapendelea Kanda ya Ziwa kama alivyozungumza Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa.
Nchemba ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma baada ya Mbunge huyo wa Iringa kuibuka hoja hiyo . Ambapo Waziri huyo amesema kuwa amekuwa Rais huyo amekuwa akisikiliza vilio vya wananchi pale anapokuwa eneo husika moja kwa moja.
“Kuna hili suala la kusema Rais anapendelea kanda ya ziwa,nataka niweke kumbukumbu sawa Mh. Rais si kwamba anapendelea Kanda ya Ziwa, ila Rais amekuwa anasikiliza vilio vya wananchi pale anapokuwa eneo husika moja ya jambo ambalo nataka nitumie kumbukumbu Mh. Rais alipokuwa Bagamoyo wananchi walipolilia eneo la Magereza alilitoa hapo hapo, huku sheria ikiwa inataka eneo lile litumike kwaajili ya Magereza,”amesema Waziri Nchemba.
“Lakini kwakuwa kilio cha wananchi kilikuwa kikubwa, na huko sio Kanda ya Ziwa ni Pwani alilitoa hapo hapo hata akusubiri maelekezo ya Wizara kukaa kama alivyosema Kanda ya Ziwa, pale aliamua hapo hapo alisema wananchi wapewe eneo hilo na hivyo ndivyo anatolea utatuzi wa changamoto za wananchi na hicho ndicho kilichomfanya achaguliwe.”
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini