Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Nenda Tu! Simba Yamtolea Uvivu Shomari Kapombe!

Katika kuonesha kwamba imeshindwa kumvumilia mchezaji wake aliesajiliwa msimu huu, klabu ya Simba imemtolea uvivu mlinzi wake Shomari Kapombe ambae kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa ni majeruhi kwa sasa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zackaria Hanspope amethibisha kuwa nyota huyo si majeruhi kwa sasa kama ambavyo taarifa zinaeleza juu ya mlinzi huyo.
Hanspope amesema kwamba vipimo huwa havidanganyi kwani vipimo vinaonesha kwamba Kapombe ameshapona isipokua uoga wake tu ndio unaomfanya kutotaka kucheza.
Mwenyekiti huyo amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa hawawezi kumsajili mchezaji kwa fedha nyingi kisha asitumike hivyo kama anahitaji kuondoka kikosini humo hawamzuii kuondoka.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App  Yetu


Android ===>  Bofya hapa
Kapombe alisajiliwa na Simba msimu huu kwa usajili huru akitokea Azam lakini hajaonekana kikosini humo tangu kuanza kwa msimu huu.
“Inategemea na yeye mwenyewe kama anataka kucheza acheze hataki aende, ni muoga tu msimamo ni yeye mwenyewe aamue kama anacheza acheze hataki aende, vipimo havidanganyi kwani vinaonesha kwamba tayari ameshapona.
“Hatuwezi kumsajili mchezaji kwa pesa nyingi halafu achezi, tumeshindwa kumvumilia, ni uoga tu,” alieleza Hanspope kwenye kituo cha redio cha efm.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017