Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Ngoma Apewa Adhabu Kali Na Klabu Yake Ya Yanga..Isome Adhabu Hiyo


Klabu ya Yanga imeamua kumuonyesha Donald Ngoma kuwa Klabu ni kubwa kuliko yeye mara baada ya kuamua kumuadhibu kutokana na Ngoma kuondoka kikosini bila kutoa Taarifa na kwenda kwao Zimbabwe.

Donald Ngoma ambaye inaelezwa kuwa amekuwa na tabia kama hiyo mara kwa mara amekatwa Dola Mia kwa kila siku ambayo hakuwepo Kikosini, Kwamujibu wa TAARIFA ZA NDANI kutoka kwa moja ya wajumbe wa kamati ya Utendaji ameiambia kwataunit.com kuwa Yanga wamemkata Donald Ngoma jumla ya Dola 2100 ambazo ni sawa na dola mia za siku 21.

Pesa hizo msomaji wetu  ni zaidi ya Milioni 4.6 za Kitanzania,  na zitakatwa kutoka kwenye mshahara wake wa mwezi wa 10.

WAKATI huohuo Klabu ya Yanga iko mbioni kumalizana na madeni ya mishahara ya wachezaji wake ambao bado hawajalipwa mishahara na Posho. Imeelezwa kuwa Yanga watawalipa wachezaji wake Malimbikizo hayo kabla ya mechi dhidi ya MBEYA CITY siku ya Jumapili November 19, 2017.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017