Kenya imeilalamikia Tanzania kwenye kitu walichokiita 'Kubadilishwa kwa sera inayobariki vitendo vya kihasama dhidi ya raia wa Kenya na biashara zao
Siku ya Jumatatu Katibu wa Mambo ya Nje na Diplomasia Tom Amollo alikosoa hatua ya Tanzania kuchoma vifaranga moto na kupiga ng'ombe mnada bila kuzihusisha mamlaka za nchi hiyo
Ameelezea kitendo hicho kinahatarisha kuchafua uhusiano mzuri uliokuwepo baina ya nchi hizo kwa muda mrefu
Hatua hiyo ilipelekea maofisa wa Kenya kumuita balozi wa Tanzania nchini humo Pindi Chana kuelezea juu ya 'maamuzi ya upande mmoja yanaoyathiri nchi zote mbili'
'Uhusiano kati ya Kenya na Tanzania ni wa muda mrefu na wenye manufaa makubwa, haufai kuhatarishwa na vitu vidogo ambavyo vinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo'' Katibu huyo aliwaambia wajumbe wa Tanzania kwenye mkutano uliofanyika Nairobi
''Kunaweza kuwa na haja ya kuwakutanisha kwa haraka maafisa wa mpakani kutoka Kenya na Tanzania kuzungumzia matatizo haya yanayojitokeza kwenye mipaka''
Pia Kenya imelaumu kuchomwa kwa vifaranga 6,400 na kwa madai ya kuenea kwa ugonjwa wa mafua ya ndege na kusema ugonjwa wa ndege haujawahi kuripotiwa Kenya
Serikali pia imesema kitendo cha kupiga mnada ng'ombe 1,325 kutoka Kenya ni
kutojali shida au maslahi ya wananchi wa Kenya walioathirika "licha ya viongozi kutoka Kenya kuomba kususbirishwa kwa zoezi hilo'
"Ufugaji katika mipaka hutokea sio tu mpaka wa Tanzania, lakini pia kwa mipaka yetu na Uganda, Sudan Kusini na Ethiopia, lakini hakuna hata mmoja kati ya nchi hizi imeamua kuchukua hatua kubwa kama hizi dhidi ya mali ya raia wa nchi jirani na rafiki'' Amollo alisema
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini