Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Yanga Wasema Watampa Adhabu Kali Donald Ngoma

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesisitiza kuwa ni lazima wampe adhabu mshambuliaji wao Mzaimbabwe, Donald Ngoma kwa utovu wa nidhamu.

Hayo, aliyasema katika mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam chini kocha msaidizi, Shadrack Nsajigwa.

Taarifa zinasema kuwa, mshambuliaji huyo aliondoka nchini na kurejea nyumbani kwao Zimbabwe bila ya kutoa taarifa kwa viongozi wake. 

Mkwasa alisema, hawana taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji huyo aliyekuwepo nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu na nusu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.

“Hatuna taarifa za kuondoka kwa Ngoma na kama ameondoka basi atakuwa kafanya makosa kwani hakutoa taarifa kwa uongozi.


“Hivyo, kama akirejea nchini na kujiunga na klabu ni lazima tumchukulie hatua za kinidhamu ikiwemo adhabu kwa kitendo alichokifanya,” alisema Mkwasa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017