Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) umesema mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006, Wema Abraham Sepetu hakuwahi kuwa mwanachama wala kukabidhiwa jukumu lolote katika operesheni za chama hicho kikuu cha upinzani kwani alikuwa shabiki.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Patrick Ole Sosopi amesema hayo juzi baada ya kutangazwa kurithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Patrobas Katambi ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi mwezi uliopita.
“Wema alikuwa shabiki wa Chadema na Chadema ina wafuasi wa namna mbalimbali. Wapo tunaowafahamu na tusiowafahamu. Wema hakuwa chochote ndani ya Chadema. Wema hakuwahi kufanya ‘movement’ yoyote. Msiwe mnasema amerudi, kwani anatoka wapi?"- Ole Sosopi.
Aliongeza; “Wema hakuwahi kupewa kadi yoyote ya Chadema. Alikuja kwa matatizo yake na ameondoka kwa matatizo yake lakini hakuwa na sifa hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Wema ameondoka peke yake, wacha waondoke".
Ole Sosopi aliyeteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha kuwa kiongozi wake, alisema kwa sasa Chadema inapitia kipindi muhimu kitakachoiimarisha.
Hata hivyo Ole Sosopi aliongeza kwamba CHADEMA wameweka mipango katika katiba kuhusiana na watu wanaohama wakitaka kurudi ndani ya chama hicho hawatakubaliwa mpaka wafanyiwe uchunguzi wa kutosha kama dhamira yao ni njema kwani wao si kama daladala ambalo unapanda, unashuka ili mradi uwe na nauli.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini