Mtangazaji wa TV, Penny Mungilwa aka VJ Penny, amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na kuimba kwenye wimbo mpya wa Diamond Platnumz, Sikomi. Penny ameiambia Dizzim Online kuwa hakuna kilichomshangaza.
“Kwanza nampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya na suala la kutoa mimba ni suala ambalo muda mrefu limekuwa likizungumziwa yaani tangu zamani linaongelewa lakini kama yeye aliona sawa kulikumbushia hakuna ubaya,” amesema Penny.
Kwenye wimbo huo Diamond anasikika akisema, ‘Achana na Penny wa hidary niliyemuhongaga gari aliponambia ana mimba Mwisho wa siku akaichomoa chali.”
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini