Mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Erick Shingongo amemnyoooshea kidole Tundu Lissu na kusema anashindwa kuelewa kwanini Mwanasheria huyo amekuwa ni mpingaji wa mambo mazuri na kusema jambo hili linamshushia heshima.
Erick Shigongo amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema yeye kwanza anapongeza hatua alizochukua Rais Magufuli juu ya sakata la madini na kudai kuwa limekuwa na matokeo chanya kwani kiongozi wa Barrick amelazimika kuja Tanzania na kubembeleza yaishe.
"Namheshimu sana Lissu, sana tu. Ni msomi wa sheria, tena mzuri tu! Lakini namshangaa, nashindwa kumwelewa kwa kitu kimoja kwamba kwa nini hawezi kukubali pale jambo jema linapofanyika? Mimi nadhani ni kujijengea heshima kubwa sana kuonyesha uzalendo pale nchi inapopambana na wizi wa maliasili ambazo hata hao Acacia wenyewe wameukubali, sasa kwa nini Lissu anaendelea kubeza kile kinachofanyika? Hakika hili linamshushia heshima" alisema Shingongo
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini