Beka Flavour kutoka Yamoto Band ameweka wazi kwamba wimbo wa kidawa wa msanii Aslay ndiyo chanzo kilichosababisha kusambaratika kwa kundi lao hadi kufikia msanii mmoja mmoja ndani ya kundi kuanza kutoa wimbo kwa kujitegemea.
Akifunguka kwenye stori tatu ya Planet Bongo ya East Africa radio, Beka amesema kuwa baada ya Aslay kutoa wimbo wa 'kidawa' ambao hakumshirikisha kiongozi hata mmoja ndani ya yamoto ikiwa pamoja na wasanii wenzake ulizua mgogoro ambao ulipelekea wasanii wengine kujiona labda hawana uwezo.
Beka Flavour mmoja wa wasanii kutoka Yamoto Band
Aidha Beka ameongeza kwamba baada ya tukio hilo la Aslay wasanii wengine ndani ya kundi hilo walilazika kuuoma uongozi uwaruhusu na wao kutoa nyimbo zao peke yao kama alivyofanya mwenzao, jambo ambalo lilipewa baraka ya viongozi tofauti na ilivyokuwa kwa Aslay.
Msikilize hapa chini Beka akifunguka kwa undani zaidi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini