Barrick Gold Corporation yenye makao yake jijini Toronto, Canada, litaunda kampuni mpya (sio Acacia) kuendesha migodi yake ya Bulyanhuru, Buzwagi na North Mara nchini Tanzania.
Katika taarifa yake juu ya makubaliano na serikali ya Tanzania yaliyofikiwa juzi jijini Dar es salaam, Shirika hilo limesema msimamo wa uwazi ulioafikiwa baina ya washirika (Tanzania na Barrick) ndio utaoainisha namna kampuni hiyo mpya itafanya shughuli zake.
"Kwa mfano Serikali ya Tanzania itashiriki katika maamuzi yahusuyo shughuli, uwekezaji, mipango, manunuzi na masoko (ya kampuni hiyo mpya itapoanzishwa)", sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Barrick Gold anayeshughulikia Shughuli za Uwekezaji na utawala Bw. Daniel Oh na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Barrick anayeshughulikia Mawasiliano Bw. Andy Lloyd.
Taarifa imesema kampuni hiyo mpya itaajili Watanzania, itawajengea uwezo wazawa katika ngazi zote, kuanzia uanachama wa bodi hadi shughuli zote, na kwamba itaongeza ununuzi wa bidhaa na huduma ndani ya Tanzania katika kuhakikisha faida ya dhahabu inaifaidisha nchi.
Taarifa hiyo imethibitisha kwamba faida ya kiuchumi kutoka katika migodi hiyo mitatu itagawanwa nusu-kwa-nusu ama 50-kwa-50 baina ya kampuni hiyo mpya na serikali ya Tanzania, faida yake ya kiuchumi ikitokana na mirahaba na kodi huku asilimia 16 ikibakia pale pale.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini