Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Lulu Atimua Mbio Mahakamani, Baba Mzazi wa Lulu Akimbizana na Waandishi wa Habari

Lulu Atimua Mbio Mahakamani, Baba Mzazi wa Lulu Akimbizana na Waandishi wa Habari

Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael (Lulu),leo baadaya kuwasili Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikiliza muendelezo wa kesi yake ya kuuwa bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Charles Kanumba. Hatimae Lulu amewakimbi waandishi wa habari waliokuwepo Mahakamani hapo huku baba ake mzazi aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakuna kupiga picha.

Tukio hilo la Lulu kuwakimbia waandishi wa habari limetokea baada ya Shahidi wa pili upande wa utetezi ambaye ni mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbushi, ambaye ameshindwa kufika mahakamani hapo leo hii kwa ajili ya kutoa ushahidi wake kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa yupo nje ya nchi na hakuweza kupatikana moja kwa moja.

Baba Lulu amekimbizana na waandishi wa habari mpaka kwenye gari analolitumia mwanae na kukaa mbele ya gari kuwaambia waandishi waliokuwepo hivi “Leo picha hampigi tafadhali mwiza maekata kata watu na viroba hampigi picha mmechimbi chini huyu mnamfuata leo hampigi picha,” hayo ndio baadhi ya maneno yaliyosikika kwa baba Lulu.

Hata hivyo mashabiki wa msanii huyo walianza kuwalaumu waandishi wa habari, kwa kusema kuwa ” Kwanini mmetuondolea Lulu wetu ilibaki kidogo aanguke na angeanguka mngempiga picha mngetukoma,” hayo ni maneno ya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo kwa waandishi wa habari.

Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba tukio linalodaiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka 2012.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017