Mbunge na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kuwajibika kuhusu kinachodaiwa kupika taarifa za serikali endapo Rais Magufuli ataruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya mwezi Julai na Agosti 2017.
Zitto Kabwe amesema kuwa wao wanatumia takwimu za serikali kuwaonyesha wananchi kuwa serikali yao inadanganya na haisemi ukweli wote na uhalisia wa uchumi na kuporomoka kwa mapato. Zitto Kabwe amedai kuwa kodi inayokusanywa na TRA nchini inaweza kulipa mishahara na kuhudumia Deni la Taifa tu na si vinginevyo.
"Kwanini Rais wetu hasemi kuwa tunakopa? Kukopa sio dhambi, kwanini aaminishe watu kuwa anatekeleza miradi kwa kuwa kodi zimeongezeka? Kama Rais anaamini kuwa mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya Julai na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi kwa umma. Rais akifanya hivyo nitawajibika" alisema Zitto Kabwe.
Jana Rais John Pombe Magufuli alisema kuwa kuna watu wanapika taarifa za serikali na kusema uongo na kuvitaka vyombo vya usalama na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kuwashughulikia watu hao ikiwezekana wafungwe kabisaa.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini