Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kocha Lwandamina Arejea Dar, Azima Taarifa Za Kujiunga Zesco

Kocha George Lwandamina amerejea nchini Tanzania na kumaliza tetesi kuwa alikuwa ameondoka katika kikosi cha Yanga kuelekea Zesco United ya kwao Zambia.
Lwandamina amerejea Dar es Salaam, alfajiri ya leo tayari kwa ajili ya kuendelea na kazi yake ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kocha huyo ataanza rasmi kazi kesho Jumatano, huku mazoezi ya leo yakiongozwa na makocha wasaidia Shedrack Nsajigwa na Mlandila kama kawaida ambao ndiyo walikuwa wakiendelea na mazoezi wakati kocha huyo alipokwenda Zambia kwa ajili ya kuhani msiba wa Mpwa wake.
>>KUSOMA HABARI NYINGI ZA MICHEZO BOFYA HAPA<<
"Kocha amerudi usiku wa kuamkia leo na kwasasa amepumzika kesho ndiyo ataanza kazi rasmi wakati leo makocha wasaidizi ndiyo wataendelea na kazi ya kukinoa kikosi kwa kufanya mazoezi ya uwanjani baada ya kumaliza mazoezi ya Gym," amesema Ten.
Msemaji huyo amesema timu yao itaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujandaa na pambano lao la Jumamosi dhidi ya Mbeya City, ambalo litapigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na wamepania kuhakikisha wanashinda.
Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 17, huku ikiwa tayari imecheza mechi 9, tangu kuanza kwa msimu huu ambao wao wakiwa mabinga watetezi wa taji hilo wanalolishikilia kwa mara 27.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017