Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

MC Pilipili Akiri Kutembea Na Mastaa Hawa


MCHEKESHAJI mahiri, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ ameweka wazi kuwa Miss Shinyanga na mshiriki wa Miss Tanzania 2014, Nicole Sarakikya na mwigizaji Rose Ndauka kwa nyakati tofauti ametembea nao lakini kwa sasa kila mtu ana maisha yake.

Pilipili alifunguka hayo hivi karibuni baada ya mwanahabari wetu kumtaka aweke ukweli juu ya warembo tofauti ambao anatajwa kuanguka nao dhambini akiwemo Nicole, Rose na msanii wa Bongo Fleva, Nandy.

“Nandy ni mshikaji tu hakuna chochote zaidi ya urafiki wa kawaida. Rose Ndauka na Nicole ni kweli nimetembea nao lakini wote siko nao kwa sasa, wamebaki kuwa marafiki wa kawaida tu,” alisema Pilipili.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017