Kiungo Mohamed Ibrahim wa Simba, ameichezea timu yake mechi ya kirafiki iliposhinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Rukwa FC.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga, Ibrahim maarufu kama Mo alionyesha kiwango kizuri kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengi waliopata nafasi.
Lakini kabla ya mechi hiyo, Mo alionekana kama ni mtu asiye na furaha.
Hata wakati Kocha Joseph Omoga akizungumza na wachezaji wote baada ya mazoezi, Mo alionekana kama si mtu mwenye furaha sana.
Hata kama atakuwa haonyeshi, lakini inaonekana Mo amekuwa hafurahii kukaa benchi jambo ambalo limekuwa likihusishw akwamba anaweza kwenda Yanga.
Hata hivyo, wakati akicheza mechi alionekana ni mwenye furaha na aliyetaka kufanya vizuri ingawa hiyo bado haifuti kwamba hawezi kuwa na furaha akiendelea kukaa benchi.
Kabla, Mo alishauriwa kuendelea kujituma na kutafuta nafasi lakini wakamshauri kuondoka ili apate nafasi zaidi ya kucheza akiwa sehemu nyingi.
Hata hivyo, Mo bado hajafungua mdomo kulizungumzia hilo na hasa suala la kuona kama anaweza kwenda Yanga ambako atapata nafasi zaidi ya kucheza.
-Salehe Jembe
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini