Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mikel Obi Aelezea Jinsi Chelsea Walivyomnyakua Toka Katika Mikono Ya Alex Ferguson

Mwaka 2005 wakati John Obi Mikel akijiunga na klabu ya Chelsea kulikuwa na mambo mengi yanayozunguka usajili huo, kubwa ikiwemo taarifa ya Obi kusaini vilabu viwili vya Manchester United na Chelsea.
Lakini Obi Mikel mwenyewe amekiri kwamba nguvu kubwa walioionesha Chelsea ikiongozwa na kocha Jose Mourinho pamoja na boss wa klabu hiyo Roman Abromovich vilimfanya kusema hapana kwa SAF.
Haikuwa rahisi kwa Obi kumtolea nje SAF kwani walikuwa na mahusiano ya karibu sana huku Fergie akimtambulisha Obi kwa manguli akiwemo Roy Keane na kumuahidi kuwa tajiri akianza kuichezea Manchester United.
Wakati Ferguson akimpa makaratasi ya awali Obi na akasaini kumbe kulikuwa na mpango wa siri wa kumnunua Obi uliokuwa ukifanywa na Chelsea huku tayari wakijua Obi anakaribia kumalizana na Chelsea.
Inasemekana wakati Obi akijiandaa kwenda Carington kumalizana na United, Chelsea walituma msafara wa magari 6 kwenda tu kumshawishi Mnigeria huyo aachane na United na asaini kwao.
Obi anakiri kwamba msafara huo ulikuwa kama wa kijeshi kwani alikuwa akipakizwa kwenye gari moja anamsikia dereva anawasiliana na walioko gari lingine kupoekea maelezo ya nini kifanyike.
Na ndipo alikutana na Jose Mourinho kwa mara ya kwanza na Jose alimuambia Obi kwamba bosi wa Chelsea anamhitaji sana kwenye timu yake na akapewa uhakika wa kupata namba katia timu ya Chelsea.
Obi anasema alivutiwa sana na Chelsea na akabadili mawazo akaamua kumtosa Ferguson jambo ambalo Obi anakiri kwamba lilimkera sana SAF kwani aliamini hakuna mchezaji ambaye angeweza kumpiga chini.
Obi anasema sio tu Chelsea waliojaribu kumuiba toka United lakini pia Barca, huku pia kuna wakala alikwenda kwake na Briefcase lenye usd 70,000 kisha akamuonesha Obi ili asaini katika klabu yake (Obi hakumbuki jina la klabu).
Obi ameitumikia Chelsea kwa misimu 11 ya ligi na kufanikiwa kushinda Champions League, Europa League, Epl mara mbili, FA Cup mara nne na kombe la ligi mara mbili na kwa sasa anakipiga Tianjin Teda ya nchini China.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017