Mwanachama wa Umoja wa Vijana wa C.C.M James Mwakibinga amezungumzia kuhusu tukio la Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kujivua uanachama na uongozi wote.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari amesema Kiongozi huyo amejivua kutokana na kushindwa na Mziki wa Rais Magufuli na kasi yake na amepoteza dila ndo sababu ya yeye kuondoka.
“Anawezejae kusema hakuna maendeleo wakati tangu Rais ameingia amefanya mambo mengi sana ya kimaendeleo yeye akubali kasi ya Rais imemshinda sasa akafungue duka la urembo na mke wake wauze uongozi hauwezi” Amesema
Aidha kaeleza kuwa wana taarifa za Nyarandu ambazo amekua anaenda Nairobi kufanya vikao vya siri na Chama pinzani na kila kitu anachokifanya habari wanayo hata saivi yupo Nairobi na akirudi ataelekea kuishi Marekani.
“Yeye anachojua kikubwa ni kupiga picha na wazungu, na kuna wenzie wawili na wenyewe tunawafanyia kazi muda ukufika tutawataja na wenyewe wana tabia kama za Nyalandu”
Amesema Nyalandu atambue pamoja na mambo aliyoyafanya hapa hatakaa kwani akiwa Waziri kuna mambo mengi aliyafanya alivumiliwa leo imefikia kunavitu anataka kuhojiwa anakimbia jambo amabalo sio zuri.
Hata hivyo amesema wanajua mpango wakke wa 2020 anataka akagombee jimbo la Arusha Mjini lakini hatoweza kwani uongozi umemshinda kitu atakachoweza afungue duka la urembo au kampuni ya Mamisi lakini sio swala la uongozi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini


