Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Tambwe Na Kamusoko Wayeyuka Mazoezini..Uongozi Yanga Watoa Tamko


Novemba 9 2017 ilitangazwa na Uongozi wa Yanga kuwa wachezaji wake Thaban Kamusoko na Amis Tambwe wangerejea katika mazoezi ya timu hiyo inayotokea mitaa ya Twiga na Jangwani lakini Jana wachezaji hao hawakuonekana katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika uwanja wa Uhuru jijni Dar Es Salaam.

Kufuatia kutoonekana kwa wachezaji hao Kwataunit.com tulifanyajitihada kuhakikisha tunapata taarifa kujua kwanini wachezaji hao hawajaonekana uwanjani . Dismas Ten mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano alisema.

Ilikuwa wafanye mazoezi leo lakini leo ni siku ya mwisho ya matibabu kama ambavyo wewe unafahamu au  daktari alivyosema kwahiyo walikwenda hospitali sehemu ambayo walikuwa wanatibiwa kwahiyo wameenda kuchukua majibu yao ya mwisho kuona kama wamepona sawasawa, kwahiyo wamepokea majibu yao na watayaleta kwa daktari wa timu na majibu rasmi yataletwa kujua ni lini wataingia uwanjani.
Yanga msomaji wa Kwataunit.com  wanajiwinda na mchezo wa raundi ya 10 ligi kuu Tanzania bara VPL dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Uhuru mchezo utakaochezwa Novemba 19.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017