Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Tunda Afungukia Mimba Yake Amtaja Mbongo Fleva Huyu Kuwa Ndo Mwenye Mzigo Wake

Tunda Sebastian
BAADA ya habari kuzagaa kwamba mrembo anayeuza nyago kwenye video mbalimbali Bongo, Tunda Sebastian kuwa na ujauzito wa staa wa Bongo Fleva, ameibuka na kufungukia ishu hiyo.

Tunda Sebastian akifanya yake na Young Dee.
Akizungumza na Star Mix, Tunda alisema hana ujauzito wa msanii huyo kama watu wasemavyo na kwamba huwa
anamuweka katika mitandao ya kijamii husan Instagram kwa sababu ya kumsapoti katika kazi zake.


“Ndiyo kwanza nasikia kwenu, siyo kweli na sina mimba yake. Huwa namuweka Insta kumsapoti kikazi tu maana ni rafiki yangu sana lakini watu walivyoona hivyo wakaanza kuzusha maneno hayo kwamba ninatoka naye na nina mimba yake. “Kuhusu kunenepa, nimenenepa kwa sababu nimeridhika na maisha mazuri niliyo nayo,” alisema Tunda.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017