Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika amesema kwamba atafanya usajili kwenye klabu yake hio kwenye dirisha dogo la usajili kutokana mapendekezo ya kocha wa timu hio, George Lwandamina.
Nyika amethibitisha kupokea maelekezo kutoka kwa kocha wake huyo kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye mzunguko huu wa kwanza kwenye kikosi hicho.
Licha kukiri kwamba kila kitu ndani ya klabu hio kinakwenda kimya kimya lakini mwenyekiti huyo amethibitisha kuwa tayari wameshaanza kazi ya kuwawinda nyota waliopendekezwa.
Usipitwe na Habari Muhimu, Install App Yetu
Android ===> Bofya hapa
Nyika pia, amesema kwamba hawezi kuweka wazi kwa sasa kama nyota wao Papy Tshishimbi atawaletea mchezaji mwingine kwenye dirisha dogo huku akisisitiza kuwa mambo yanakwenda kimya kimya.
“Nitafanya usajili wa Young Africans dirisha dogo kwa maelekezo ya George Lwandamina. Tayari amekwisha nieleza wapi mapungufu yapo na mimi na jopo langu tumeanza kazi rasmi kuteleza mahitaji yake ili kuiboresha timu kiufundi . Kila kitu kinakwenda kimya kimya “alisema Nyika.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini


