Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

VIDEO::Mama Kanumba Aangua Kilio Baada Ya Lulu Kuhukumiwa Kwenda Jela Na Kunena Mazito

Mwigizaji Elizabeth Michael “Lulu” leo amehukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia na kusababisha kifo cha Mwigizaji Steven Kanumba.
Baada ya Hukumu hiyo kutolewa Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba aliangua kilio na kuongea yafuatayo >>> “Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano
Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani” – Mama Kanumba

Mtazame Mama Kanumba mwenyewe kwenye hii video hapa chini
Credit:Millard Ayo

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017