Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Joshua Nassari adai kutishiwa kuuawa, avamiwa Usiku na watu wenye bunduki

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amedai usiku wa kuamkia Jumamosi hii alivamiwa na watu wasiojulika wakiwa na bundiki na kufyatua risasi nje ya nyumba yake.

Nassari amedai muda mchache baada ya tukio hilo yeye pamoja na mke wake walifanikiwa kufika kituo cha polisi na kutoa ripoti ya tukio hilo.

“Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu,” alitweet Nassari.

Amedai watu hao baada ya kufyatua risasi walifanikiwa kumuuwa mbwa wake ambaye alikuwa nje ya nyumba.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara.
Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi.
Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu.




Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017