Mwanadada Mange Kimambi ameibukia sakata la Wema Sepetu kurudi CCM,ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu atabiri mpango wa Wema Kurudi CCM.
Akizungumza kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Kimambi amesema Wema hajawaangusha watanzania pekee bali amejiangusha yeye mwenyewe kwa kutokua na msimamo.
“Hujawaangusha waTZ tu, umejiangusha mwenyewe pia, your fans and everyone who cared for you. Hivi kizazi hiki kina Winnie Mandela hakuna kabisa eehe? Nakuonea huruma mnoooo sababu umepoteza credibly yooooote kwenye jamii”Ameandikia Mange Kimambi.
Hivi karibuni Mange alisema kuwa anazo taarifa za uhakika kuwa Wema Sepetu pamoja na Mama yake watarudi chama cha Mapinduzi akidai kuwa mama yake amekubali kurudi isipokuwa anasuburiwa yeye.
Mange alisema mpango wa kurudi CCM unafuatia Wema na Mama yake kubanwa katika mambo mbalimbali kutokana na kuwa upande wa upinzani.
Wakati akitangaza kurudi CCM jana Wema alisema..
“Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani… Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani” . Wema Sepetu.
Wema alijiunga chama cha Chadema mwezi februari mwaka huu akitokea chama cha Mapinduzi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini