Kiungo mshambuliaji wa Difaa Al Jadida ya Morocco, Simon Msuva amempa tano straika wa Yanga, Ibrahim Ajibu kwa kusema yupo vizuri na kusema uwezo wake utaisaidia klabu yake kutetea ubingwa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Msuva ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, alisema Ajibu hadi sasa amefanya vizuri katika timu yake kutokana na kiwango anachokionyesha katika mechi tisa za ligi alizocheza hadi sasa.
Yanga ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi hiyo, kwa sasa ipo nafasi ya tatu katika ligi kuu ikiwa na pointi 17 nyuma ya Azam FC yenye pointi 19 katika nafasi ya pili huku Simba ikiwa kileleni na pointi 19 pia lakini ina uwiano mzuri wa mabao.
Msuva amesema kiwango kinachoonyeshwa na Ajibu kinaleta matumaini ya Yanga kuendelea kutetea ubingwa wao msimu huu licha ya ushindani uliopo.
“Ajibu ni mchezaji mzuri naamini uwepo wake na ushirikiano na wachezaji wengine utaisaidia Yanga kutetea ubingwa wao iwapo watajituma kwa pamoja.
“Kwa jinsi nilivyoona msimamo, ligi inaonekana ni ngumu kwa kuwa timu hazijapishana sana kwa pointi, hivyo wachezaji wa Yanga wanatakiwa kumsikiliza kocha na kujituma ili kupata matokeo mazuri,”
alisema Msuva.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini