KA T I K A mechi mbili za mwisho za Simba katika Ligi Kuu Bara zilizochezwa hivi karibuni, Shiza Kichuya ameifungia timu yake mabao mawili, huyu amekuwa mchezaji muhimu kikosini kwa sasa.
Kichuya alifunga bao katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga halafu wikiendi iliyopita aliifungia Simba bao pekee na la ushindi katika mechi dhidi ya Mbeya City ambapo S i m b a ilishinda bao 1-0.
Bao dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya limemfanya Kichuya kufikisha mabao matano sawa na yaliyofungwa na Ibrahim Ajibu wa Yanga, mwenyewe anafurahia na anataka kuongeza kasi zaidi.
Kichuya amefanya mahojiano na Championi Jumamosi, na hii ni sehemu ya mahojiano hayo;
KUNA UTATA WA BAO LAKO ULILOIFUNGA MBEYA CITY, SIYO OFFSIDE ILE?
“Lile ni bao halali kabisa kwani kama lingekuwa na utata mwamuzi pamoja na wasaidizi wake wangelikataa lakini kwa vile halikuwa na tatizo lolote ndiyo maana walilikubali.
“Hayo yanayosemwa kuwa nilikuwa nimeotea kabla ya kufunga wala hawaniumizi kichwa, jambo la msingi nilifunga na mwamuzi alilikubali bao hilo, kwa hiyo sikuotea kama wanavyodai.
UNA MABAO MATANO, HII IMEKAAJE?
“ N i n a s h u k u r u Mungu kwa hilo kwani msimu huu kuwa na mabao hayo si mchezo, ligi ni ngumu kwani kila timu imejiandaa vilivyo ukilinganisha na msimu uliopita.
“Namwomba Mungu aendelee kunijalia afya njema kila siku ili niweze kuitumikia timu yangu kwa mafanikio m a k u b w a pia niweze kufunga mabao mengi z a i d i y a haya niliyonayo sasa.
U N A M A B A O S A W A NA AJIBU, U N A M C H U K U LIAJE?
“ K u s e m a kweli najisikia vizuri kwa hilo kwani Ajibu ni mmoja kati ya wachezaji ambao ninawaheshimu sana.
“Ajibu siyo mtu wa mchezomchezo anajua anachofanya anapokuwa uwanjani, ana uamuzi wake wa haraka ambao huifaidisha timu yake na yeye ni mtu muhimu kwa timu yake.
“Yule si mtu mzuri kwani anaweza kubadili matokeo muda wowote ule, hivyo kulingana mabao na mtu kama yeye ni jambo zuri.
“Lakini ninachoweza kusema ni kwamba mimi sishindani naye katika ufungaji ila nacheza soka kwa ajili ya kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri uwanjani.
“Ikitokea nimefunga namshukuru Mungu pia akifunga mwingine na kuiwezesha timu yetu kupata ushindi pia n a f u rahi, kwa hiyo Ajibu ni mchezaji mzuri na ninamheshimu lakini sishindani naye kwa ufungaji.
UMEIFUNGA YANGA MARA TATU MFULULIZO, HII UNAIZUNGU3MZIAJE?
“Siyo Yanga tu ambayo nimeifunga mara tatu hata Mbeya City nayo nimeifunga mara tatu.
“Kwa hiyo hakuna kitu k i n g i n e a m b a c h o ninaweza kusema juu ya hilo ila inatokea tu, inawezekana yakawa ni maajabu ya soka tu.
YULE MTOTO UNAYEINGIA NAYE U W A N JANI NI NANI?
“Yul e m t o to ni shabiki y a n g u amb a y e anavutiwa na aina ya uchezaji wangu kwa hiyo kutokana na thamani anayonipatia basi na mimi huwa namthamini kwa kuwa naye uwanjani.
K I C H U Y A NI JINA LA UKOO WAKO AU LA UTANI?
“Kichuya ni jina la ukoo wetu na siyo la utani kama watu wanavyofikiria, jina langu halisi ni Shiza Ramadhani Kichuya.
UME F U N GA MECHI MBILI MFUL U L I Z O NINI AHADI YAKO?
“Siwezi kutoa ahadi yoyote kuhusiana na kuendelea kufunga ila ninachoweza kusema ni kwamba namuomba Mungu anijalie afya njema ili niendelee kuitumikia Simba.
“Nitaitumikia Simba kwa nguvu zangu zote ili msimu huu tuweze kufanya vizuri. Ikitokea nikafunga katika mechi zinazokuja basi nitafurahi pia.
UBINGWA VIPI?
“Ni mapema sana kuzungumzia suala zima la ubingwa kwa sababu ligi bado ipo mwanzoni lakini msimu huu ligi ni ngumu sana ukilinganisha na uliopita.
“Msimu huu mpaka sasa timu inayoongoza katika m s i m a m o , i n a o n g o z a kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa pia timu z ime z i d i a n a pointi chache sana, kwa hiyo suala la ubingwa siyo sawa kulizungumzia kwa sasa,” anasema Kichuya.
MSIMAMO WA WAFUNGAJI
E.Okwi Simba 8
M.Rashid Prisons 6
I.Ajibu Yanga 5
S.Kichuya Simba 5
E.Ambokile Mbeya 4
H.Haji Mbao 4
M.Boniventure Majimaji 3
O.Chirwa Yanga 3
M.Yusuph Azam 3
Ve.Ludovick Kagera 3
A.Kwasi Lipuli 3
-GPL
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini